Watuhumiwa wa madawa ya kulevya wakiwa wamekamatwa
Mtuhumiwa aliyekuwa akisafirisha madawa hayo kutokea Tanga kwenda Dar akiwa chini ya ulinzi wa Polisi
Huyu yeye alikuwa na gari ndogo akiwa anasindikiza mzigo huo, walikamatwa baada ya Polisi kuwa wakiwafwatilia nyendo zao zote.
Haya ndiyo madawa yenyewe yakiwa kwenye sanduku yalimokuwa yakisafirishwa kwenda Dar
Polisi hapa wanastahili pongezi kwa kuweza kuzuia haya madawa ambayo yangeleta mathara makubwa kwa jamaa na ndugu zetu wengi
Hii habari ya madawa ya kulevya ilitokea juma mosi tarehe 23/07/2011 majira ya saa kumi na moja jioni eneo la Kabuku, Tanga.
Kulikuwa na abiria (jina halikupatikana) kwenye basi la Raha Leo lilikuwa likitoka Tanga kwenda Dar. Basi lilisimamishwa na askari pale Kabuku na kuamurishwa kuingia kituoni. Askari Kanzu wawili waliingia kwenye basi na kuanza kukagua, wakaenda moja kwa moja kiti cha mwisho, wakamuuliza abiria mmoja kama ana tiketi, na wakaamuru ashuke. Alipoulizwa kama ana mzigo, alikataa, lakini kondakta alikumbuka kwamba abiria huyo aliweka sanduku kwenye boot. Ndipo alikubali kwamba ana mzigo lakini sio wake, ametumwa na watu (wahindi wawili) awapelekee Dar, wenyewe wana kuja na gari dogo. Sanduku hilo lilikuwa na takribani kilo kumi na mbili (12) za cocaine iliyokadiriwa kuwa na thamani ya Tsh.720m.
Kulingana na taarifa walizokuwa nazo polisi, Wahindi wawili (mwanamme na mwanamke) wenye umri unaodairiwa kuwa kati ya miaka 30 na 35 waliokuwa wametangulia kwa gari dogo aina ya Toyota ........... Walikamatwa Kabuku kabla ya basi haijafika. Na basi lilipofika, yule abiria aliyekutwa na madawa ya kulevya aliwatambua kuwa ndio waliomtuma. Wahindi hao walikana madai na kusisitiza kwamba hawamjui abiria huyo. Wahindi wawili na abiria huyo walitiwa nguvuni hapo kabuku ili kusubiri taratibu zingine zifuate.
Ni matumaini yetu kuwa watu hawa wamefunguliwa mashitaka na haki itachukua mkondo wake.