Ujasiriamali na Kilimo cha Mbono
>> Wednesday, August 3, 2011 –
Ujasiriamali
Kilimo cha zao la mbono (Jatropha) sasa ni mkombozi kwa wananchi wa Mpanda. Ni kama ndoto, lakini huo ndio ukweli halisi kwamba Watanzania tuna raslimali nyingi sana ambazo zinaweza kututoa kimasomaso kiuchumi kama tutaamua kufanya kazi kwa bidii na maarifa na kuwa wabunifu.
Shamba la Mibono |
Zao la miti ya mbono kwa wakazi wa maeneo ya Mpanda mkoani Rukwa,limekuwa sasa mkombozi kwa wananchi wa kipato cha chini, hali illiyompelekea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mizengo Pinda kuwaunga mkono wanachi hao ambao sasa wanazalisha mafuta na sabuni yenye dawa kutokana na zao la mbono.
Mti huu umeweza kuwatoa kimasomaso na kujikuta wakipata mafuta ya taa na dizeli kwa matumizi ya kuendeshea matrekta madogo maarufu kama power tiller.
Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda alifikia uamuzi huo wa kusaidia jumla ya shillingi milioni thelathini (30,000,000) kwa vikundi vya wakulima wa Mpanda ili vijikwamue kwa kutumia teknlogia hiyo rahisi na inayotunza mazingira. Uzinduzi wa mradi wa kukamua mafuta ya dizeli kutoka kwenye mbono ulifanyika mwaka jana wakati wa mbio za mwenge wilayani hapo ambapo mafuta hayo yaliweza kujazwa kwenye magari yaliyokuwa kwenye msafara wa mbio za mwenge.