Inawezekana. Powered by Blogger.
Showing posts with label Ujasiriamali. Show all posts
Showing posts with label Ujasiriamali. Show all posts

Kula Mboga za Asili kwa Afya Yako

Shirika lisilo la kiserikali la RESEWO limeanzisha bustani ya maonyesho ya mboga za asili ya Tanzania. Bustani hii iko ndani ya Kijiji cha Makumbusho, Dar es Salaam.


Mboga za asili zina faida nyingi kiafya, na hata huweza kutumika kama tiba mbadala kwa magonjwa mbalimbali.

Kishona nguo

 Kishona nguo huweza kutumiwa kama mboga, kama juisi na pia kama kiungo cha chai. Inaongeza damu mwilini, inaondoa uchovu na husaidia kuzuia magonjwa mbalimbali.

Mchicha maua
Delega

Juisi ya Kishona guo
... unaweza hata ukaotesha mboga ndani ya ndoo

Afisa Utawala na Masoko wa Resewo, Bi. Stella Muro akiwa ofisini

Read more...

Nyumbu Ndani ya Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma

Maonyesho ya wiki ya utumishi wa umma yalifanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam kuanzia tarehe 16/06/2011 hadi tarehe 23/06/2011.

Moja kati ya vivutio vingi vilivyokuwepo kwenye maonyesho hayo, yalikuwa ni magari ya Nyumbu yanayotengenezwa hapa nchini na taasisi ya Tanzania Automotive Technology Centre, iliyoko Kibaha, Pwani. Taasisi hii inamilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

  
Lori la Nyumbu

Licha ta magari, TACT pia hutengeneza mashine mbalimbali kama mashine za kutengeneza matofali, pump za maji na trailers.









Vipuri vya mitambo

Read more...

Ujasiriamali na Kilimo cha Mbono

Kilimo cha zao la mbono (Jatropha) sasa ni mkombozi kwa wananchi wa Mpanda.  Ni kama ndoto, lakini huo ndio ukweli halisi kwamba Watanzania tuna raslimali nyingi sana ambazo zinaweza kututoa kimasomaso kiuchumi kama tutaamua kufanya kazi kwa bidii na maarifa na kuwa wabunifu.

Shamba la Mibono

Zao la miti ya mbono kwa wakazi wa maeneo ya Mpanda mkoani Rukwa,limekuwa sasa mkombozi kwa wananchi wa kipato cha chini, hali illiyompelekea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mizengo Pinda kuwaunga mkono wanachi hao ambao sasa wanazalisha mafuta na sabuni yenye dawa kutokana na zao la mbono.

Mti huu umeweza kuwatoa kimasomaso na kujikuta wakipata mafuta ya taa na dizeli kwa matumizi ya kuendeshea matrekta madogo maarufu kama power tiller.

Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda alifikia uamuzi huo wa kusaidia jumla ya shillingi milioni thelathini (30,000,000) kwa vikundi vya wakulima wa Mpanda ili vijikwamue kwa kutumia teknlogia hiyo rahisi na inayotunza mazingira. Uzinduzi wa mradi wa kukamua mafuta ya dizeli kutoka kwenye mbono ulifanyika mwaka jana wakati wa mbio za mwenge wilayani hapo ambapo mafuta hayo yaliweza kujazwa kwenye magari yaliyokuwa kwenye msafara wa mbio za mwenge.

Unaweza kupata maelezo ya kina zaidi kuhusiana na mradi wa zao la mbono huko Mpanda katika Jarida la Inawezekana toleo la mwezi Juni 2011

Jengo la Mradi wa DISAT huko Mpanda

Read more...

About This Blog

  © Blogger template Shush by Ourblogtemplates.com 2009

Back to TOP