Gari laanguka maeneo ya kawe katika mazingira yasiyoeleweka
Gari likivutwa kutoka eneo la tukio baada ya kuanguka katika mazingira ya ajabu hakuna mtu aliyeumia au kufa.
Read more...
Uzinduzi wa Kilimo kwanza Promosheni SumaJkt
Mh Affan O. Maalan Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Maliasili Zanzibar akizindua promosheni ya bahati nasibu ya SumaJkt Jijini Dar es salaam leo.
Meza kuu ya Waheshimiwa na viongozi wengine akiwemo Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Maj General Samweli Kitundu, Mkurugenzi Mkuu SumaJkt Col. Ane Mwakang'ata, Mwenyekiti wa Bodi ya SumaJkt Maj General Ligate Sande (Rtd). Kwenye uzinduzi wa shinda Matrekta na zawadi nyingine nyingi.
Mgeni Rasmi akiwa amemaliza kukata utepe kuashiria kuanza kwa promosheni hiyo
Read more...
UZINDUZI WA BAHATI NA SIBU YA KILIMO KWANZA NA SUMAJKT
kikundi cha ngoma kikijiandaa kwaajili ya kutumbuiza
maafisa masoko wakiwa tayari kwa sherehe
Maandalizi ya High Table
Matrekta na Power tiller zinazoshindaniwa
Uzinduzi wa Promosheni kabambe ya kushinda Matrekta, Power tiller na Pesa Taslim
iliyoandaliwa na SUMAJKT Agri machinery Project at Mwenge (Lugalo Area) Read more...
Paul na Lilian Wameremeta huko kwenye mji wa Kusoma
Paul Mhando na Mkewe Lilian
Bibi Harusi akiwasili Kanisani kwa ajili ya siku yao na wapambe wakiwa tayari kumsindikiza ndani.
Bibi Harusi akisindikizwa na Bw Daniel Semwenda kumkabidhi kwa Bw Harusi
Bw na Bi Harusi wakiwa wamesimama wakisubiri wakati uwadie
Bw na Bi Harusi wakiwa wamekaa wakifuatilia kwa karibu.
Bwana harusi akimwangalia mkewe kweli umekuwa wangu sasa!
Bw na Bi D Semwenda pamoja na Bi harusi
Picha pamoja na Mchungaji na Mkewe mwenyekiti wa Cite uk
Mc akiwa anatambulisha upande wa Bi harusi
Paul anahakikisha details zote ziko sawa
Wageni waalikwa wakiwa wanaburudika na vinywaji
Raph in the house doing His ting
Read more...
Watuhumiwa wa madawa ya kulevya wakiwa wamekamatwa
Mtuhumiwa aliyekuwa akisafirisha madawa hayo kutokea Tanga kwenda Dar akiwa chini ya ulinzi wa Polisi
Huyu yeye alikuwa na gari ndogo akiwa anasindikiza mzigo huo, walikamatwa baada ya Polisi kuwa wakiwafwatilia nyendo zao zote.
Haya ndiyo madawa yenyewe yakiwa kwenye sanduku yalimokuwa yakisafirishwa kwenda Dar
Polisi hapa wanastahili pongezi kwa kuweza kuzuia haya madawa ambayo yangeleta mathara makubwa kwa jamaa na ndugu zetu wengi
Hii habari ya madawa ya kulevya ilitokea juma mosi tarehe 23/07/2011 majira ya saa kumi na moja jioni eneo la Kabuku, Tanga.
Kulikuwa na abiria (jina halikupatikana) kwenye basi la Raha Leo lilikuwa likitoka Tanga kwenda Dar. Basi lilisimamishwa na askari pale Kabuku na kuamurishwa kuingia kituoni. Askari Kanzu wawili waliingia kwenye basi na kuanza kukagua, wakaenda moja kwa moja kiti cha mwisho, wakamuuliza abiria mmoja kama ana tiketi, na wakaamuru ashuke. Alipoulizwa kama ana mzigo, alikataa, lakini kondakta alikumbuka kwamba abiria huyo aliweka sanduku kwenye boot. Ndipo alikubali kwamba ana mzigo lakini sio wake, ametumwa na watu (wahindi wawili) awapelekee Dar, wenyewe wana kuja na gari dogo. Sanduku hilo lilikuwa na takribani kilo kumi na mbili (12) za cocaine iliyokadiriwa kuwa na thamani ya Tsh.720m.
Kulingana na taarifa walizokuwa nazo polisi, Wahindi wawili (mwanamme na mwanamke) wenye umri unaodairiwa kuwa kati ya miaka 30 na 35 waliokuwa wametangulia kwa gari dogo aina ya Toyota ........... Walikamatwa Kabuku kabla ya basi haijafika. Na basi lilipofika, yule abiria aliyekutwa na madawa ya kulevya aliwatambua kuwa ndio waliomtuma. Wahindi hao walikana madai na kusisitiza kwamba hawamjui abiria huyo. Wahindi wawili na abiria huyo walitiwa nguvuni hapo kabuku ili kusubiri taratibu zingine zifuate.
Ni matumaini yetu kuwa watu hawa wamefunguliwa mashitaka na haki itachukua mkondo wake.
Subscribe to:
Posts (Atom)