Inawezekana. Powered by Blogger.

Mazingira Yetu Tuyatunze

 Hapa ni karibu na hospitali ya Ocean Road kulikuwa na miti mikubwa sana eneo hili. Sasa wamejenga nyumba kubwa tu ndiyo ni maendeleo lakini kwanini wasingeacha baadhi ya miti ambayo kwa kweli ingeongeza kivutio pamoja na majengo mapya? Lete maoni yako wewe jinsi unavyoona.
 Inawezekana kubadili mtazamo wetu katika mazingira. Inawezekana tukawa na maendeleo na tukawa na mazingira mazuri pia. Inawezekana tukabadili fikra zetu na tukawa tunaangalia na vizazi vijavyo tunawaachia mazingira gani? Inawezekana kuwa na mazingira Bora.

Kwa mbali kule unaona mabaki ya miti ambayo imetolewa katika eneo hili. Naamini kuwa wangeweza kujenga hivyo wanavyojenga lakini miti hiyo ikiwepo humo na watu wakaegesha magari yao kwenye vivuli vya miti hiyo na kuleta madhari nzuri pia. Wana mazingira mpo vitu kama hivi mnasemaje? Toa maoni yako katika blog hii ili kujaribu kuyawakilisha kwa wahusika.

Post a Comment

About This Blog

  © Blogger template Shush by Ourblogtemplates.com 2009

Back to TOP