Inawezekana. Powered by Blogger.

Wezi wa Nyaya za Umeme Tanzania

 Huyu yeye alikuwa anaiba nyaya huko upanga, alikufa mlangoni mwa hospitali ya Muhimbili




Kama inavyoonekana hapo kwenye pembe ya chini.

Read more...

Mazishi ya Mchina

 Hii ni picha ya Mchina mmoja aliyefariki Jijini Dar hivi karibuni na misa yake kufanyika maeneo ya kurasini karibu na ofisi za uhamiaji makao makuu.

 Barabara ya kuelekea uhamiaji ilikuwa imefungwa wakati wa misa hiyo ambayo waliifanya katikati ya barabara.


Umati wa watu wajamii ya wachina wakiwa katika misa hiyo maeneo ya kurasini

Read more...

MKUTANO WA MASHETANI

Jitahidi usome mpaka mwisho kuna kitu muhimu utajifunza. Toa mawazo yako unavyoona



MKUTANO WA MASHETANI
Lucifer, Mkuu wa mashetani  aliitisha semina elekezi kwa mashetani wote Duniani na katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano
huo alisema:-

"Tumeshindwa kuwazuia WANADAMU wasiende kwenye nyumba
za IBADA" Tumeshindwa kuwazuia wasisome VITABU vyao vitakatifu na kufahamu ukweli"
Tumeshindwa hata kuwazuia wasiwe na mapenzi ya kweli kwa MITUME yao " "Mara wapatapo muungano wa kweli kwenye MAHUBIRI ya DINI zao, mamlaka yetu yatakuwa yamefika mwisho."
Kwa hiyo kuanzia sasa waacheni waende kwenye nyumba zao za IBADA, waacheni waendelee na karamu zao za upendo,
LAKINI waibieni muda, ili wasipate nafasi ya kudumisha IBADA za kweli kweli kwa MOLA WAO MUUMBA...." 

"Hiki ndicho ninachotaka mfanye." Alisema Lucifer:
"wataabisheni WANADAMU WOOTE wasipate kamwe kushikamana na DINI zao na wasifungamane katika KUMCHA MUNGU" 
"
Tutafanyaje jambo hilo?" mashetani yalimwuuliza
kwa jazba.
LUCIFER aliwajibu:"hakikisheni wanakuwa 'BUSY' (BUSY= Being Under
Satan's York ) katika mambo yasiyokuwa na umuhimu katika
maisha yao na muwanzishie mipango mingi sana isiyohesabika ili
kujaza akili na ufahamu wao. "Washughulisheni na kutumia, na kutumia, na kutumia; na kukopa, nakukopa, na kukopa."
”Washawishini wake zao waende kufanya kazi kwa siku na kushinda huko kwa masaa mengi sana kwa siku na Waume
zao wafanye kazi kwa siku sita hadi saba kwa wiki, na masaa
10 hadi 12 kwa siku, ili wasiweze kupata nafasi ya kutulia na kutafakari chochote kulingana na mfumo huo wa maisha." "Wazuieni wasiwe na nafasi ya kukaa na watoto wao" 

"Wachocheeni zaidi akili na fahamu zao ili kuhakikisha
kwamba hawaiskii ile sauti ndogo tulivu ya Mungu wao." 
"Washawishini walize radio au kaseti au muziki kwenye simu,
popote wanapoendesha gari au wanapotembea kwa miguu.
Waache TV,VCR, CD na KOMPYUTER zikiwa zimewashwa kama kawaida majumbani mwao na mhakikishe kwamba kila duka na mgahawa kote duniani linapiga muziki usiokuwa wa KIDINI
tena mfululizo bila kukoma."  "Hii itasonga akili na fahamu zao
na kuvunja ule muungano kwa MOLA WAO."

"Jazeni magazeti na vijarida mbalimbali vya upuuzi kwenye
meza zao za kahawa na chai Duniani kote."

"Shindilieni habari na matukio mbalimbali ndani yafahamu zao
kwa muda wa masaa 24."  "Ingilieni kwenye muda wao wa
kuendesha barabarani kwa kuwaonyesha mabango na matangazo.'  "Kwenye masanduku ya posta na barua pepe jazeni vipeperushi
na majarida na kila aina ya matangazo ya habari za vitu na hudumu yanayowapa matumaini ya uongo."
"Wekeni wanawake warembo sana mitaani, club, maofisini  na kwenye Televisheni na majarida ili kwamba Wanaume walioko kwenye ndoa wadanganyike na kuamini kwamba urembo wanje ndio muhimu, na wasiridhike na wake zao."

"Wafanyeni wake zao wachoke sana wasiweze kuonyesha
upendo kwa waume zao nyakati za usiku.Wapeni maumivu
ya kichwa ili wasiwape waume zao upendo wanaouhitaji
sana,ili waanze kutazama kwingine. Wafanyeni Wanawake wawadharau Waume zao na kuwapuaaza.
"Hiyo itaparaganyisha familia zao haraka sana !
 
"Wapeni WANADAMU Waalimu wa uongo ili wawapotoshe wasifundishe maneno ya MUNGU ya kweli kwa watoto wao
na waumini wao." 
"Hakikisheni wanakuwa 'BUSY' na kusongwa na mambo kiasi kwamba hawapati muda wa kutafakari wema wa Mungu. Badala
yake wapeni kutalii kwenye maeneo ya ajabu, matukio ya
michezo, matamasha, kumbi za sinema na video."Wafanye wawe 'BUSY,' 'BUSY,' 'BUSY,! Yaani wasongwe na kusongwa na
kusongwa na kazi kwelikweli!" 
 
"Na wanapokutanika kwenye ibada zao za kiroho wafanye
waingie katika umbea na fitina na kuzungumzia  mambo
madogo madogo ya umbea na fitina ili waondoke wakiwa na dhamira mbaya zilizochafuliwa." 
"Jazeni visababishi vingi vya mambo katika maisha yao ili
wasiwe na nafasi ya kutafuta msaada na nguvu za MUNGU.
Muda si mrefu watakuwa wakitegemea akili zao wenyewe,
badala ya maelekezo ya MUNGU, huku wakihatarisha afya
zao na za familia zao kwa ajili ya maangamizi  yao wenyewe."
 "Itafanya kazi"  "Itafanya kazi!
"Huu ni mkakati kweli kweli. Mashetani yaliondoka kwenye
mkutano yakiwa na hamu kubwa sana ya kutekeleza majuku
hayo waliyopewa na kuanza kuwafanya WANADAMU wawe
wa kukimbia na mambo huku na huko. Watakuwa na muda
mdogo sana kwa ajili ya Mungu wao na familia zao. Wakakosa
muda wa kuwaeleza wengine kuhusu MAMBO YA IBADA na
kubadili maisha ya wanadamu.
NADHANI SWALI NI JE SHETANI AMEFANIKIWA
KATIKA MIPANGO YAKE HIYO? WEWE NDIYE HAKIMU !!!!!!!!
 
'UBIZE' au kutingwa na kazi kunamaanisha : kuwa chini ya mkataba au utumwa wa shetani?
PLEASE PASS THIS ON, IF YOU AREN'T TOO BUSY !!

Read more...

Baada ya kutoa jino usiogope kutabasamu maana ni mwanya wa pembeni tu.

Read more...

ahah

Read more...

Njaa inatoka wapi?

Watu wakiosha karoti zao kwenye mto Karanga. Unawezakuona jinsi Tanzania tulivyobarikiwa na vitu vingi lakini bado nchi ni masikini sana. Hapo hapo ukiwa mjini Dar na maeneo mengine unaweza kuona magari ya kifahari sana na majumba ya kifahari sana na hapa huwa najiuliza umasikini wetu uko wapi sasa? wadau wengine unafikiri vipi?


Nyumba za wafanyakazi wa TPC Moshi, tangu enzi ya Mwl Nyerere lakini mpaka leo zinaonekana vizuri. Ukina nyumba zilizojengwa sasa na sirikali ya hivi karibuni zimechakaa kuliko za zamani je tunakwenda mbele au tunarudi nyuma?

Read more...

Kilimo cha Umwagiliaji


Bw Michael akiwa shambani mwake ambako anafanya kilimo cha umwagiliaji. Inawezekana kwa vijana wakarudi na kufanya shughuli za kilimo na kufanikiwa zaidi kuliko kufanya biashara za uchuuzi mjini na huku wakiwafaidisha zaidi wale wenye maduka. Huku wao wakiwa wamezunguka kwenye jua sana. Maoni yako mdau Bw Peter na Dr Lusingu

Read more...

Mvule wa Ajabu

Kibao kilichoko kwenye Mvule wa ajabu una Upana wa mita tatu (3) urefu wa kutoka chini mpaka kwenye tawi la kwanza ni mita 30 na urefu wake ni mita 51. Unakisiwa kuwa na miaka zaidi ya 191.

Read more...

 Kilimo cha umwagiliaji pembeni ya mto njiro, Wanapata mpunga mwingi tu kama tungeweza na kuyatumia hayo maji hapo chini kwa ajili ya umwagiliaji Tanzania ingeondokana na tatizo la kuagiza chakula kutoka nje. Ilitakiwa sisi ndiyo tuwe watu tunaotegemewa kwa chakula Afrika.

Read more...

Gate la kuingia kwenye msitu wa njiro. Lakini angalia hayo matakataka hapo pembeni

Read more...

Daraja la Karanga Tangu Mwaka 1939

Daraja la Karanga, Zamani lilikuwa ndiyo linaunganisha kati ya Moshi na Arusha. Ilikuwa barabara kuu, limejengwa na Waitaliano mwaka 1939 - 1945. Angalia daraja lilivyo imara kwa miaka yote hiyo. Wenye maelezo zaidi tunaomba tuletee.

Read more...

Mti wa Mlonge



 Raisi Mstaafu wa Msumbiji akipata maelezo kutoka kwa wadau wa miti ya milonge huko Bagamoyo
 Majani ya Mlonge yakiwa yameanikwa kwenye chumba chenye giza ili isipoteze ubora wake kwa ajili ya kusagwa na kutoa unga ambao unaweza kutumiwa kwa matumizi mbali mbali.
 Wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Makai Moringa (Mlonge) Enterprises ya Dar es salaam

Read more...

Rais Mstaafu wa Msumbiji Mh J. Chisano alipotembelea mashamba

 Rais Mstaafu Joachim Chisano akikaribishwa kwenye kijiji cha Kikaro kata ya Miono wilaya ya Bagamoyo hivi karibu kuangalia kilimo cha miti ya Mlonge.

 Hapa Rais Mstaafu akiwa anakagua shamba la miti hiyo.
Akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa kilimo cha miti ya milonge na wazalishaji wa bidhaa za Mlonge. Mlonge ni mti ambao majani yake unaweza kutumia kama mboga na dawa pia mbegu zake kwa ajili ya mafuta yakula na pia kama dawa. Mizizi yake hutumika kama dawa. Ni miti yenye faida nyingi sana na unatibu magonjwa mengi.

Read more...

Arusha Maeneo ya Njiro

 Sehemu ya makazi kwa kutokea kwenye jengo la Esami
 Eneo la viwanda Njiro na sehemu ya makazi
Mount Meru Kwa mbali inavyokuwa imefunikwa na mawingu na chini ni maeneo ya njiro upande wa viwanda

Read more...

Kitega Uchumi cha Kanisa

Read more...

PATA HABARI

Sasa unaweza
kutuma maoni,
maswali na
kupokea habari
za uwekezaji,Biashara
pamoja na kilimo.
TUMA NENO INAWEZEKANA KWENDA NAMBA
15522.
          

Read more...

Mruma Secondary School (Mruma Girls)

 Kamera yetu ilifanikiwa kufika katika hii shule na kuwajulia hali baada ya kuondoka eneo hilo miaka mingi sana iliyopita. Haya kwa wale mliosoma hapo miaka mingi iliyopita. Rose K kipindi hicho ukiwa unatumia jina hilo. Upo lete maoni yako.



 Enzi hizo sehemu hii mlikuwa mnaita vipi?

 Hall letu hilo sasa je kipindi hicho ilikuwa nini?
 Computer Room mambo yanaendelea secondary zote ziwe na vyumba kama hivi jamani karne ya 24 bado. Tusaidie shule zile ambazo tulizosoma. Wadau mnasemaje?
 Kitambulisho cha shule
Haya vijana wa sasa mliacha nembo zenu je mnakumbuka? Angalia kama yakwako bado ipo.

Read more...

Ulaji wa Nyama choma yenye latha

Imenikumbusha Nilipokuwa kijana ikifika wakati wa kwenda kijijini wakati wa sherehe mnakuwa mnachoma nyama na kula kiasi unachotaka.




Read more...

About This Blog

  © Blogger template Shush by Ourblogtemplates.com 2009

Back to TOP