Inaendelea No 2
aliyepo akinitazama. Wakaniona jinsi nilivyobadilika toka unyonge na kuwa mwenye furaha.
Nilikuwa natabasamu, narukaruka na kuimba.
Picha wakimwombea:
Maxima:
Binti yangu ghafla akawa mwenye furaha ndani ya moyo na kuanza kula. Alionja karibia kila kitu
kilichokuwepo, huku akisema, “Kama sitarudi, sawa nimeshakula na kushiba.”
Angelica:
Kila mmoja akaanza kucheka na kuuliza, “kwanini uko hivyo badala ya kuwa na huzuni, unafuraha
na mwenye raha?” nikawajibu, “Ndiyo ninafuraha: ninakwenda kumwona Bwana, nitakuwa naye,
lakini sijui kama nitarudi. Kwa hiyo nataka kugawa vitu vyangu vyote.” Wote wakastaajabu na
kuniuliza, “Unataka kugawa vitu vyako vyote?” macho ya mama yangu yalinitazama kwa
mshangao zaidi!
Maxima:
Binti yangu akaanza kugawa vitu vyake. Aligawa vyote, vyote! Ma-dada wa kanisani walikuwepo,
nao pia aliwapa baadhi ya vitu kwa kila mmoja. Nilipomuuliza nia yake, alisema, “Kama nikirudi,
watanirejeshea vyote, lakini nisiporudi, watabaki navyo.”
Angelica:
Niliwaza huzuni aliyokuwa nayo mama yangu niliposema maneno hayo. Lakini nilijisikia furaha
tupu, kwa hiyo nikaendelea kugawa vitu: nguo, kitanda, simu ya mkononi, kila kitu, lakini kwa
sharti: kama nikirudi, kila kitu kitarejeshwa kwangu. Wote wakaanza kucheka.
Maxima:
Binti yangu alikuwa na msimamo na nia ya dhati, lakini kama mama nilishikwa na huzuni sana.
Haikuwa jambo rahisi. Niliwaza, “Bwana muda huo ukiwadia, itakuwajekuwaje?” Sikuweza
kuelewa. Na walipoanza kuomba, nilikuwa napanga vitu ndani ya nyumba. Walisema, “Dada njoo
tuombe.” Lakini niliwajibu, “Nyie endeleeni, nitajiunga nanyi muda si mrefu. Ngoja nimalizie kazi
hii.”
Angelica:
Wote walikuwa wananiangalia mimi tulipokuwa tunaomba. Niliomba, “Bwana, nataka kufanya
mapenzi yako. Wewe si mwanadamu hata useme uwongo au ujute, najua wewe ni mkweli. Kama
nitakuaibisha, basi vema unichukue moja kwa moja; lakini kama nitayafanya mapenzi, basi
unirejeshe tena, lakini nisaidie kusema ukweli, niandae mimi, nisaidie kuhubiri na kuwaambia watu
kutubu.” Hiyo ndiyo ilikuwa sala yangu fupi sana. Nilimwambia mtumishi wa Bwana,
6
“Usimwambie mama yangu maneno niliyomwomba Bwana.” Naye akajibu, “sitamwambia sasa,
lakini mara Bwana atakapokutwa, nitamwambia.” Tuliendelea kuomba na kuungana katika duara.
Maxima:
Ilipofika saa 9:30 jioni, Bwana akamwambia mtumishi wake ampake mafuta binti yangu. Kwa hiyo
baadhi yetu tulikwenda chumbani na kumpaka mafuta. Alitupa dakika mbili tumpake mwili mzima,
toka kichwani hadi chini, kila mahali, mwili mzima. Akawa mwili wote amepakwa mafuta.
KIFO CHAKE
Angelica:
Mama yangu na dada mmoja, Fátima Navarrete, walinipaka mafuta. Kadri walivyokuwa
wananipaka, nilijisikia kama kuna kitu kinanifunika, kama kioo kilinizunguka mimi. Ni vigumu
kuelezea, nilijisikia kama nimezingirwa na ngao fulani, na nashindwa kuelezea nilivyokuwa
najisikia. Baada ya hapo kila walipojaribu kunigusa walishindwa!
Maxima:
Kadri tulivyokuwa tukimwombea Angelica, nilijaribu kuweka mkono juu yake, nilishindwa!
Alikuwa amezingirwa na kitu. Ilikuwa ajabu, hakuna aliyeweza kumgusa tena! Uzio huo ulianzia
kichwani hadi miguuni, karibia sentimenta 30 (Inchi 12). Hilo lilinitisha zaidi mimi. Nimewawekea
mikono wengi kabla, katika huduma ya Bwana, lakini jambo kama hili halijawahi kutokea!
Nikasema, “Oh, kuna jambo lazima linatendeka,” na nikaanza kuomba na kumshukuru Bwana.
Ghafla, nikasikia furaha kubwa sana. Huzuni iliyokuwa moyoni ikanitoka, maumivu yakakoma na
sasa nikasikia raha na furaha ajabu! Tuliendelea kuomba na ilipofika saa 10.00 jioni, binti yangu
akaanguka sakafuni.
Angelica:
Wakati wa maombi, nilisikia kuishiwa pumzi; nikashindwa kupumua. Nikasikia maumivu tumboni
na moyoni. Nilijisiki damu ikisimama, na ghafla maumivu makali mwili mzima. Nililoweza
kusema, “Bwana, nipe nguvu, nipe mimi nguvu!” kwasababu nilijisikia kushindwa kuendelea zaidi.
Sikuwa na nguvu kabisa, zote zilinitoka! Na nilipoangalia juu mbinguni, katika roho, si kwa macho
ya mwilini, niliona mbingu zikifunguka. Niliwaona malaika, siyo wawili au kumi, bali kwa
mamilioni wakiwa pamoja wamekusanyika. Katikati yao niliona mwanga, mara 10,000 zaidi ya
jua. Na nikasema, “Bwana ni wewe unayekuja!”
Maxima:
Alipoanguka chini, tulijaribu kumsimamisha, lakini hakuweza kusimama mwenyewe. Muda huu
tuliweza kumgusa. Alikuwa akisema, “Omba. Sina nguvu, mama, sina nguvu na ninasikia
maumivu.” Mwanzo alisikia maumivu tumboni, na baadaye moyoni. Tuliendelea kuomba na
kumsihi Bwana. Bwana alichukua maisha yake!
Picha Mwili wake:
7
Sijawahi katika maisha yangu kumwona mtu akifa. Nilishuhudia binti yangu, akigugumia maumivu! Haikuwa rahisi hata kidogo! Sikuweza kuelewa maneno yake ya mwisho, na mwisho alitulia. Niliweka mikono yangu usoni pake, na kioo mdomoni kuona kama alikuwa anapumua. Hakuwa na pumzi tena, alitulia kimya kabisa. Nilimshika, alikuwa angali na joto kama kawaida. Nilichukua shuka na kumfunika na kwa muda mfupi akaanza kupoa na kuwa wa baridi sana. Nywele zake zikalala, kama za maiti na akabadilika ubaridi wa barafu.
Angelica:
Yesu alikuwa anashuka chini, na nikajisikia mwili ukifa. Kadri Yesu na malaika walivyozidi kukaribia, nikajisikia kuondoka, na sikuwa mimi tena. Sikuwa hai tena, nilikuwa nakufa na kugugumia maumivu! Wakati mwili wangu ulipoanguka chini, walikuwa tayari wamefika. Nyumba yetu ilijaa malaika, na katikati yao niliona mwanga mkali kuliko wa jua! Ilikuwa vigumu; nilisikia maumivu makali wakati roho yangu ilipotenganishwa na mwili. Nilikuwa nalia na kupiga kelele, kadri nilivyoona mwili wangu sakafuni. Nilimuuliza, “Bwana, nini kinachotokea? Nini kinachotokea?” Nilijaribu kuugusa mwili wangu na kuurudia tena, lakini nilipojaribu, ilikuwa kama kushika hewa: sikuweza kuugusa, mkono wangu ulipitiliza. Hakuna kati ya waliokuwa wananiombea aliyenisikia! Na nikapiga kelele, “Bwana, nisaidie mimi!”
Maxima:
Mume wangu alifika tulipokuwa tunaomba, na alimkuta pale. Bwana alinipa nguvu kwa kuwa sikujua la kufanya. Ilikuwa kama vile yuko mahututi (kwenye coma), lakini nilijua yuko salama, kwasababu ilikuwa ni kazi ya Bwana. Kwahiyo nikasema “Bwana, mapenzi yako yafanyike.”
BWANA YESU KRISTO
Angelica:
Wakati huo nasikia sauti ya Bwana, sauti nzuri kama radi lakini ya UPENDO, “Usiogope, Binti, kwa kuwa mimi ni Yehova, Mungu wako, na nimekuja hapa kukuonesha niliyokuahidi wewe. Inuka, kwa kuwa mimi ni Yehova, ninayekushika mkono wako wa kuume na kukuambia, usiogope, nitakusaidia wewe." Ghafla, nikasimama. Nilikuwa nimepiga magoti chini, ninauangalia mwili wangu, nikitaka kuurejea bila mafanikio. Niliposikia sauti yake, woga ukanitoka, na sikuwa na hofu tena. Nilipoanza kutembea, malaika wakaanza kufungua njia. Kulikuwa na mwanga mkali ung’aao, na nilipouangalia nilisikia amani ya ajabu. Kadri nilivyoangalia, nilimwona mwanaume mzuri, mrefu, aliyevaa vizuri na kuvutia sana kumwangalia, mwenye siha njema. Mwanga ulitoka kwake. Kulikuwa na mwanga mkali kiasi cha kushindwa kumwangalia uso wake! Lakini niliweza kuona nywele zake za dhahabu ing’aayo na vazi jeupe na mshipi kifuani pake. Ukisomeka, “MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA.”
Nilimwangalia miguuni pake, alikuwa amevaa sandozi zenye mng’ao wa dhahabu, dhahabu safi. Alikuwa mzuri sana! Akaninyooshea mkono wake. Nilipomshika mkono wake, haikuwa kama nilipojaribu kuugusa mwili wangu, mkono haukupitiliza. Nikauliza, “Nini kinachotokea?” naye akasema, “Nitakuonesha wewe kuzimu ili ukirudi uwaambie wanadamu kuwa kuzimu ni halisi; kuwa ni kweli ipo. Na pia utukufu wangu nitakuonesha wewe, ili uwaambie watu wangu wajiaandae, kwa kuwa utukufu wangu ni halisi na mimi pia.” Akasema, "Binti, usiogope” akarudia kusema tena na mimi nikasema, "Bwana, nataka tu kwenda Mbinguni, lakini siyo kuzimu, kwasababu nimesikia kunatisha!” Akasema, “Binti, nitakuwa nawe. Sitakuacha huko na nitakuonesha huko mahali kwasababu wengi wanajua kuzimu ipo lakini hawaiogopi.

Itaendelea