Tuendelee Kujifunza vitu vinavyoweza kusaidia katika Maisha
James 2:17 In the same way, faith by itself, if it is not accompanied by action, is dead. Read more...
11
wakikumbuka kuwa walimjua Mungu, kwasababu walijua neno. Walimjua Bwana waliteswa mara
dufu ya wengine.
Bwana akasema, “Hakuna tena nafasi kwa walioko pale[kuzimu]; kungali na nafasi kwa walio
hai.” Nikamuuliza, “Bwana, kwanini bibi yangu mkubwa yupo pale? Sijui kama alikujua wewe.
Kwanini yupo kuzimu Bwana?” akanijibu, “Binti, yupo hapa kwasababu alishindwa
kusamehe….. binti, yeyote asiyesamehe, sitamsamehe huyu.”
Nikamuuliza, “Bwana, lakini wewe husamehe, na una rehema.” Naye akanijibu, “Ndiyo, binti,
lakini nilazima kusamehe, kwasababu hawajawasamehe wengi, na ndiyo maana wengi wapo
hapa, wameshindwa kusamehe…… nenda kawaambia wanadamu ni muda wa kusamehe, hasa
hasa watu wangu, kwakuwa wengi miongoni mwa watu wangu hawajasamehe. Waambie
waache malaaumu, mafundo, chuki mioyoni mwao, kwa kuwa ni muda wa kusamehe! Kama
kifo kikimsitukiza mtu aliyeshindwa kusamehe, huyo mtu atakwenda kuzimu, kwakuwa hakuna
awezaye kununua maisha.” Tulipoondoka hapo, bibi yangu mkubwa alifunikwa na moto na
akapiga makelele, "Aaaah," na akaanza kutukana jina la Mungu, na kumlaani Bwana; kila mtu
kuzimu humtukana Mungu.
Tulipoondoka eneo lile, nikaona kuwa kuzimu imejaa roho ziteswazo. Watu wengi huinua mikono
nje, wakimwomba Yesu msaada wa kuwatoa nje. Lakini Bwana hakuwa na lolote la kufanya kwao,
nao huanza kumtukana Mungu. Mara Yesu hulia sana na kusema, “Inaniumiza sana kuwasikia,
inaniumiza mimi sana wanavyofanya, kwasababu siwezi kufanya lolote kwaajili yao. Ninacho
kueleza ni hiki; nina nafasi kwa hao walioko duniani, ambao hawaajafa, walio hai, wanao muda
wa kutubu!”
Bwana akaniambia kuna watu wengi maaruku huku kuzimu, na pia wengi waliomjua Bwana.
Akasema, “Nitakuonesha upande mwingine wa tanuru.” Tukaenda mahali penye mwanamke
aliyezingirwa na miali ya moto. Alikuwa katika maumivu makubwa na kupiga makelele, akiomba
huruma kwa Bwana. Yesu akanyoosha mkono kwake na akaniambia, “Binti, Yule mwanamke
umwonaye pale, amezingirwa na miali ya moto ni Selena.” Kadri tulivyokuwa tunamkaribia,
akapiga kelele, “Bwana, nihurumie mimi, nisamehe mimi Bwana, nitoe mahali hapa!” lakini
Bwana akamtazama na kusema, "Umechelewa, umechelewa sana, huwezi kutubu sasa.”
Selena
Aliponiona mimi akasema, “Tafadhari, nakuomba wewe, waambie watu hivi, tafadhari sema na
usinyamaze; nenda waambie wasije mahali hapa; nenda waambie wasisikilize nyimbo zangu, wala
wasiimbe hizo nyimbo.”(1 Yohana 2:15) Nikamuuliza, "kwanini unataka mimi niwaambie hivyo?"
12
naye akanijibu, "Kwasababu kila wakati watu wanaposikiliza nyimbo zangu, nateswa zaidi na
zaidi, na mtu anayeimba na kusikiliza nyimbo zangu, anaelekea mahali hapa. Tafadhari, nenda
uwaambie wasije huku; nenda waambie kuzimu ni halisi, ipo kweli!”. Akapiga kelele na mapepo
humchoma mikuki na Selena kulia, “Nisaidie mimi, nihurumie mimi Bwana!” lakini kwa huzuni
Bwana alimwambia, “umechelewa sana.”
Nikaangalia pande zote za eneo lile, lilikuwa limejaa waimbaji na wasanii waliokufa. Walikuwa
wakiimba na kuimba, bila kusimama. Bwana akanifafanulia, “Binti, mtu aliyepo hapa, lazima
aendelee kufanya kile alichokuwa anafanya duniani, kama hajatubu."
Kadri nilivyokuwa naangalia eneo lile, niliona mapepo mengi yakinyunyiza vitu kama mvua.
Nilidhani ni mvua inanyesha. Lakini niliona watu kwenye miali ya moto wakikimbia mbali na ile
mvua na kupiga yowee, “Hapana, nisaidie, Bwana!..... Hapana, haiwezekani kuwa hivyo,” na
mapepo yalikuwa yanacheka na kuwaambia watu, “Sifu na kuabudu kwasababu hapa ni ufalme
wenu milele na milele!” Niliona miali ya moto ikiongezeka na funza za watu zikiongezeka zaidi!
Hayakuwa maji yale bali kiberiti cha kuongeza miali ya moto na kuongea maumivu ya kila mtu.
Nikamuuliza Yesu, “Ni nini kinachotokea?..... Bwana, ni nini hiki?” Bwana akanijibu, “Huu ni
ujira wa yeyote asiyetubu.” (Zaburi 11:6).
Bwana akanipeleka mahali alipo mtu aliyejulikana sana. Kabla ya maono haya, nilishi maisha kama
msichana wa kikristo wa nia mbili. Nilidhani kila mtu anayekufa anakwenda Mbinguni; wale
walifanyiwa ibada za mazishi watakwenda mbinguni, kumbe sikuwa sahihi, nilikosa. Alipofariki
Papa John Paul II, marafiki zangu na ndugu walisema amekwenda mbinguni. Taarifa zote kwenye
LUNINGA [TV], na vyombo mbalimbali vya habari vilisema, "Papa John Paul II amefariki,
apumzike kwa amani. Anafurahia sasa kuwa na Bwana na malaika Mbinguni" na mimi niliamini
yote kuwa ndivyo. Lakini kumbe nilikuwa najidanganya mwenyewe, kwasababu nimemwona
kuzimu, akiteswa kwa miali ya moto. Nilimtazama uso wake, alikuwa mwenyewe Papa John Paul
II! Bwana akaniambia, “Angalia, Binti, Yule mwanaume umwonaye pale, ni Papa John Paul II.
Yuko hapa; akiteswa kwasababu hakutubu.”
Papa John Paul II
Lakini nikamuuliza, “Bwana, kwanini yuko hapa? Alikuwa akihubiri kanisani.” Yesu akanijibu,
“Binti, hakuna mwasherati, wala muabudu sanamu, hakuna mchoyo na hakuna mwongo
atakayerithi ufalme wangu.” (Eph 5:5) Nikamjibu, “Ndiyo, najua ni kweli, lakini nataka kujua
kwanini yuko hapa, kwasababu alikuwa akiwahubiria umati wa watu!" Na Yesu akanijibu, “Ndiyo,
Binti, alisema mengi, lakini hakusema kweli kama ilivyo. Hakusema kweli na kweli aliijua na
japokuwa aliijua kweli, alipenda fedha zaidi ya kuhubiri habari za wokovu. Hakutoa uhalisia;
hakusema kuzimu ni halisi na mbinguni kupo; Binti, sasa yuko mahali hapa."
13
Nilipomwangalia mtu huyu, alikuwa na joka kubwa lenye sindano nyingi mwilini mwake, limemzingira shingoni, naye hujaribu kumtoa. Nalimwomba Yesu, “Bwana, msaidie!” Mwanaume hupiga kelele, “Nisaidie mimi, Bwana nihurumie; nitoe mahali hapa; nisamehe mimi! Ninatubu Bwana; Nataka nirudi duniani, nataka nirudi duniani nikatubu.” Bwana alimtazama na kumwambia, “Ulijua vizuri yote haya. Ulijua vema kuwa kuzimu ni halisi, ipo…….. umechelewa; hakuna tena nafasi kwaajili yako.”
Bwana akasema, “Tazama Binti, nitakonesha maisha ya mtu huyu.” Yesu akanionesha kioo kikubwa kama LUNINGA [TV]; nikaona alivyotoa misa mara nyingi kwa umati wa watu. Na watu wale walivyokuwa waabudu sanamu. Yesu akasema, “Tazama, Binti, wapo waabudu sanamu wengi hapa [Kuzimu]. Ibada ya sanamu haiwezi kuokoa Binti. Ni mimi pekee niwezaye kuokoa, na nje yangu hakuna mwingine aokoaye. Nawapenda wenye dhambi, lakini nachukia dhambi Binti. Nenda na uwaambie wanadamu kuwa nawapenda na ninataka waje kwangu.”
Kadri Bwana alivyokuwa akisema, nilianza kuona mtu huyu akipokea makusanyo makubwa ya sarafu na fedha; vyote alivihifadhi. Alikuwa na fedha nyingi sana. Naliona sura yake imeketi katika mamlaka yake, lakini pia naliweza kuona zaidi. Japo ni kweli watu hawa hawaoi, ninakuhakikishia wewe, sizushi, Bwana alinionesha mimi, wanalala na masista; na wanawake wengi!
Bwana akanionesha watu hawa wanaishi kwa uasherati, na neno linasema hakuna mwasherati atakayerithi ufalme wake. Kadri nilivyokuwa naona, Bwana akaniambia, “Tazama, Binti, yote ninayokuonesha, ndiyo yanayoendelea, ndivyo alivyoishi [Papa] na ndivyo yanayotokea katikati ya watu wengi, katikati ya mapadre na mapapa waliopo.” Kisha Bwana akasema, “Binti, nenda na uwaambie wanadamu ni muda wa kugeukia.”
Bwana akanionesha sehemu watu wengi wanavyoelekea kuzimu. Nikamuuliza, “Bwana, namna gani wanakuja huku?” akanijibu, “Nitakuonesha.” Akanionesha lango lenye watu wengi wakipita. Watu hawa walikuwa wamefungwa toka mikononi hadi miguuni. Walivaa mavazi meusi na kubeba mizigo mgongoni mwao. Yesu akasema, “Binti, hao watu uwaonao hawanijui mimi bado. Mizigo waliyobeba ni dhambi, lakini nenda waambie walete mizigo kwangu, nami nitawapumzisha; kwa kuwa mie ndiye mwenye kusamehe dhambi zao zote…. Binti, nenda na uwaambie waje kwangu, kwani nawasubiri na mikono yangu iko wazi kuwapokea, na uwaambie hapo wanaelekea mahali hapa [kuzimu].”
Kadri nilivyokuwa nawatazama watu wakitembea, nikamwambia, “Bwana, Yule mtu pale ni binamu yangu; na Yule kijana pia, Bwana, na Yule binti pale anayelekea kuzimu; oh familia yangu inakuja huku kuzimu!” Bwana akajibu, “Binti, wanakuja huku, lakini nenda uwaeleze wanakoelekea, nenda waeleze kuwa wanakwenda kuzimu. Nenda waeleze kuwa nimekuchagua wewe uwe mlinzi wangu…… nimekuchagua wewe kama mlinzi, hii inamaanisha kuwa unatakiwa uwaambie ukweli. Unatakiwa uende uwaeleze yote niliyokuonesha wewe. Kama hutawaambia na jambo likampata mtu huyu, damu yake itakuwa juu yako, lakini ukiende na kufanya nilivyokueleza, hapo mtu huyu nitamdai mwenyewe. Kama mtu hatatubu, hapo wajibu ulionao utaondolewa, kwa kuwa atadaiwa mwenyewe na damu yake haitakuwa juu yako. (Ezekia 3:18)"
Yesu akaniambia wengi wa watu maarufu wanaelekea huku [kuzimu], maarufu na watu muhimu. Kwa mfano, Michael Jackson. Huyu alikuwa maarufu duaniani kote lakini alikuwa mjumbe wa
14
shetani. Japokuwa wengi wanaweza wasione na kuelewa hivyo, lakini huo ndiyo ukweli. Huyu
alikuwa na mkataba na shetani: alikubaliana na shetani ili awe na heshima na sifa ilikuwa vutia
wapenzi wengi.
Michael_Jackson
Hizo hatua na mitindo aliyokuwa anafanya, ndivyo nilivyoona mimi mapepo yakicheza na
kutembea yanapotesa watu kuzimu. Yalikuwa yanateleza kwa kurudi nyuma na siyo mbele, huku
yakipiga kelele; yakifurahia mateso wanayopata watu. Ngoja nikuambia wewe kuwa Michael
Jackson yuko kuzimu. Bwana alinionesha baada ya kufa Michael. Alinionesha Michael Jackson
akiteswa kwenye miali ya moto. Nikalia kwa Yesu, “Kwanini?” haikuwa rahisi kuona mtu huyu
alivyokuwa anateswa na alivyokuwa analia na kupiga mayowe. Yeyote anayesikiliza nyimbo za
Michael Jackson au kuziimba au ni mpenzi/shabiki wa Michael Jackson, ninakuonya kuwa shetani
anakutega katika mtego wake ili mwisho uishie kuzimu. Mara hii, jitoe na kumkana shetani kwa
jina Yesu! Yesu anataka kukuweka huru wewe, ili usipotee milele. Bwana akaniambia, “Binti,
kuna watu wanijuao pia wanakuja huku.” Nikamuuliza, “Bwana, inakuwa je mtu akujue harafu
aje huku?” akanijibu, “Mtu Yule aliyeacha njia zangu na mtu Yule anayeishi aina mbili za
maisha [wokovu na dhambi].” Akaanza kunionesha watu wanaoelekea kuzimu. Walikuwa
wamefungwa kamba toka mikononi hadi miguuni. Kila mmoja alivaa vazi jeupe, lakini
limetobokatoboka, lina-mabakamabaka na limekunjamana. Yesu akaniambia, “Binti, angalia watu
walioniacha mimi. Binti, nataka kukueleza, siji duniani kwaajili ya watu hawa. Nakuja kwaajili
ya watakatifu, waliotayari, wasiolaumiwa, wasio na makunyanzi na wasio na mawaa…… nenda
uwaambie warejee kwenye njia zao za zamani,” (Efeso 5:26-27) Nilianza kuwaona wengi
miongoni mwa wajomba zangu na watu wengine wengi waliorudi nyuma na kuziacha njia za
Bwana. “Nenda kawaambie ninawasubiri, walete mizigo yao nami nitawapumzisha." YESU
alikuwa analia baada ya kusema hayo, “Binti, wanakuja huku [kuzimu]. Nenda kawaambie
wajomba zako; nenda kawambie ndugu zako kuwa wakuja huku! Binti, wengi hawatakuamini,
lakini mimi ni shahidi wako mwaminifu, ni shahidi wako mwaminifu. Sitakuacha wewe. Hata
kama hawataamini, Binti, nenda na uwaambie ukweli huu, kwa kuwa nipo nawe. Pia Binti
nitakuonesha jinsi watu wanavyofika huku.”
Tulikwenda kwenye lango, ambapo tuliona umati wa watu wakiangukia ndani ya shimo kubwa.
Siyo elfu moja wala elfu mbili, bali wingi wake kama mchanga wa bahari, hawana idadi!
Walikuwa wananguka kwa kila sekunde, mfano wa mkono uliojaa mchanga umwakikapo chini.
Zile roho zilikuwa zinaanguka kwa kasi. YESU alikuwa akilia, na kusema, “Binti hivi ndivyo
wanadamu wanavyopotea; hivi ndiyo mwanadamu apoteavyo!!!..... Binti, inaniumiza sana mimi
nionavyo wanadamu wanavyoangamia.”
YESU akasema, “maapepo pia hufanya mikutano huku.” Na nikasema, “mapepo yanafanya
mikutano?” Yesu akasema, "Ndiyo, Binti, wanakutana kupanga, kupanga watavyowafanya
wanadamu. Wanakutana kila siku kwa siri.” Na kwa hilo, Yesu akanipeleka kwenye sero,
15
ambapo niliona meza ya mbao na viti vikizunguka meza. Na palikuwa na mapepo, aina zote za
mapepo. Yesu akaelezea, “Binti, wanapanga kwenda kuharibu nyumba/familia za wachungaji,
wamisionari, wainjilisti na wote wanijuao mimi. Binti wanataka kuwaharibu; wanamishale
mingi.”
Mapepo hucheka na kudhihaki, na kusema, “acha tuwaharibu wanadamu na kuwaleta huku.” Yesu
akasema, “Nenda na uwaambie nipo pamoja nao watu wangu. Waambie wasiache milango wazi,
wasimpe nafasi shetani, kwa kuwa shetani anazunguka-zunguka kama simba angurumaye,
akimtafuta wa kummeza. (1 Petro 5:8)" Lakini neno linasema, "anatembea kama", kwasababu
simba halisi, ni Simba wa Yuda, Yesu Kristo wa Nazareti (Ufunuo 5:5)! Yesu akasema, "Binti,
wanataka kuharibu/kuangamiza familia za wachungaji.” Nikamuuliza, “Kwanini wanataka
kuharibu familia za wachungaji?” na Yesu akajibu, “Kwasababu wanawajibu wa maelfu ya watu
ambao ni kondoo wa kundi; kondoo wa kundi Bwana aliowakabidhi wao. Wanataka watu hao
warudie dunia tena; waangalie nyuma na kuishia kuzimu…. Nenda kawaambie wachungaji
kusema iliyo kweli tupu. Waeleze wahubiri kweli tupu na kusema kila kitu ninachowaambia na
wasinyamaze nayo haya ninayowaambia!”
Tulipokuwa tunaondoka hapo, akaniambia, “Nataka nikuoneshe kitu kingine…. Wapo pia watoto
huku.” Na nikamjibu, “watoto huku Bwana? Kwanini wawepo watoto huku? Neno lako lasema,
'Waacheni watoto wadogo waje kwangu, na msiwazuie: kwa maana Ufalme wa Mbinguni ni wao."
(Mathayo 19:14) Yesu akajibu, “Binti, ni kweli, ufalme wa mbinguni ni wao, lakini mtoto lazima
aje kwangu, kwa kuwa kila ajaye kwangu sitamtupa kamwe." (Yohana 6:37) Ghafla, Bwana
akanionesha mvulana wa miaka nane akiteswa kwenye moto. Mvulana akalia, “Bwana nihurumie
mimi, nitoe mahali hapa, sitaki kuwepo hapa!” aliendelea kupiga kulia na kelele. Nikaona mapepo
yamemzunguka mtoto huyu, yaliyofanana na cartoon. Kulikuwa na aina za Dragon, BoyZ, Ben 10,
Pokémon, Doral, na nyingine nyingi. “Bwana, kwanini mtoto huyu yuko huku?" Yesu akanionesha
picha ya mkanda wa maisha mtoto huyu. Nilimwona anavyotumia muda karibia wote kwenye
LUNINGA [TV] akiangalia cartoon.
Cartoon ya Ben 10: Pokemon:
Yesu akasema, "Binti, hayo maigizo ya cartoon, sinema zake, michezo mbalimbali ya kuigiza
inayooneshwa kila siku kwenye LUNINGA [TV] ni vyombo vya shetani atumiavyo kuwaharibu
wanadamu….. tazama, binti ilivyotokea kwa mtoto huyu." Nilimwona jinsi mtoto huyu
alivyokuwa mkaidi na asiye mtii kwa wazazi wake. Wazazi wake aliposema naye alikimbia na
kutupatupa vitu ovyo na kuto-watii. Baada ya hapo akagongwa na gari na ukawa mwisho wa
maisha yake. Yesu akasema, “Tangu hapo yupo mahali hapa.”
Nilimtazama mtoto Yule akiteswa. Yesu akasema, "Binti, nenda na uwaambie wazazi
wawaelekeze watoto wao kama ilivyo katika neno langu.”(Mithali 22:6) Neno la Mungu ni halisi,
16
linatuambia tumwonye mtoto kwa fimbo, lakini si kila wakati, pale tu mtoto anapoonyesha ukaidi
kwa wazazi. (Mithali 22:15)
Bwana akaniambia kitu cha kuhuzunisha sana na kuumiza mno. Akasema, “Binti, wapo watoto
wengi sana huku kwasababu ya cartoon, kwasababu ya ukaidi.” Nikamuuliza, “Bwana, kwanini
lawama ziwe hizi cartoon?” Naye akanieleza, “Kwasababu ni mapepo yanayobeba ukaidi, kiburi,
ukali na chuki kwa watoto, ili wasifanye vitu vizuri; na mapepo mengine huwaingia watoto ili
wasifanye mambo mazuri, bali wafanye mabaya: vile waonavyo kwenye LUNINGA [TV] watoto
hutaka kufanya vivyo hivyo.” Kuzimu ipo, kuzimu ni halisi, na watoto lazima waamue
watakwenda na nani. Nikasema, “Bwana, niambia, kwanini kuna watoto huku?” na Yesu akanijibu,
“Mara watoto wapatapo kujua kuna mbinguni na kuzimu, hapo wanayonafasi ya kuchagua.”
UFALME WA MBINGUNI
Kuna mengi ya kusema juu ya kuzimu, lakini kwasasa niwashirikishe niliyoyaona Mbinguni. Yesu
akasema, "Binti, sasa nitakuonesha nilichowaandalia watakatifu wangu.” Tuliondoka kule
kuzimu kupitia lango lake. Tulipokuwa tukisafiri kutoka nje ya kuzimu, ghafla tukatokea mahali
penye mwanga. Sikuona giza tena, mateso wala miale ya moto. Akasema, “Binti, nitakuonesha
utukufu wangu,” na tukaanza kupanda juu kwenda Ufalme wa Mbinguni! Mara tukafika kwenye
mlango wenye maandishi makubwa yaliyoandikwa kwa dhahabu, yalisema: “Karibu
kwenye Ufalme wa Mbinguni.”
LANGO LA MBINGUNI
Yesu akasema, “Binti, ingia, kwa kuwa mimi ni Mlango na kila aingiaye kupitia kwangu,
ataingia na kupata marisho.”(Yohana 10:9)
Baada ya Bwana kusema maneno hayo, mlango ukafunguka na tukaingia. Niliwaona malaika
wakimpa utukufu, heshima na sifa Baba Yetu wa Mbinguni! (Ufunuo 7:11-12) Kadri tulivyozidi
kutembea, tulikaribia meza niliyoweza kuona mwanzo wake laini siyo mwisho. (Ufunuo 19:9)
Niliona enzi kubwa, na enzi ndogo zimezungukwa na maelfu ya viti. Katikati ya viti niliona mavazi
na mataji. Bwana akaniambia, “Binti, taji unayoiona pale ni taji ya Uzima."(Ufunuo2:10)
Yesu akasema, “Tazama, Binti, hii ndiyo niliyowaandalia watu wangu.” Niliona ile meza
imefunikwa na vitambaa vyenye upindo wa dhahabu. Kulikuwa na sahani, glasi za dhahabu,
matunda; kila kitu kimeandaliwa. Ilikuwa nzuri ajabu. Kulikuwa na chombo kikubwa katikati ya
meza, kilichokuwa na mvinyo tayari kwa mulo. Na Yesu akasema, “Binti, kila kitu kipo tayari kwa
ujio wa kanisa langu.”
17
MEZA YA KARAMU YA MBINGUNI
Tulikwenda mahali pengine, niliwaona watu wengi wakiwa bustanini. Kulikuwa na watu
wanaofahamika sana kwenye Biblia, lakini hawakuwa wazee, bali vijana. Palikuwa na kijana akiwa
na kitambaa mkononi, akicheza na kuzungukazunguka na kumsifu Bwana. Yesu akasema, “Binti,
Yule kijana pale ni mtumishi wangu Daudi.” Alikuwa akimpa utukufu Baba yetu. Ghafla, kijana
mwingine akapita na Yesu akaniambia, “Binti, huyu ni Joshua; Yule Musa; na Yule pale ni
Ibrahimu.” Yesu huwaita kwa majina yao. Wote walikuwa na mwonekano mmoja! Ajabu sana
Mbinguni! Yesu akasema, “Mwanamke Yule ni mtumishi wangu, Maria Magdalena; na Yule
mtumishi wangu Sara."
Lakini pia akaniambia, “Binti, huyu ni Maria. Maria, aliyemzaa Yesu Kristo, ambaye ni mimi.
Binti, nikwambie, yeye hana habari ya yanayotokea duniani. Nataka kukwambia, nenda
kawaambie wanadamu, waambie waabudu sanamu kuwa kuzimu ni halisi, na waabuduo
sanamu hawata urithi Ufalme wangu, lakini waambie kama wakitubu, wataweza kuingia makao
ya mbinguni. Nenda waambie nawapenda na pia waambie Maria hajui chochote
[kinachotendeka duniani] na pekee wanayeweza kuheshimu ni mimi, kwasababu si maria wala
mtakatifu Gregory wala mtakatifu yeyote awezaye kuokoa. Mimi ndiye niokoaye na nje yanguhakuna
yeyote, hakuna yeyote, hakuna yeyote – aokoaye!” Alirudia mara tatu-kuwa hakuna
yeyote awezaye kuokoa; isipokuwa yeye.
Wanadamu wamedanganywa na kuamini kuwa kwa kupitia wadhaniwao ni watakatifu, sivyo
ilivyo, bali ni mapepo, yafanyayo kazi kupitia sanamu zilizofanywa kwa mikono ya watu. Lakini
ngoja nikueleze kwamba Bwana anataka kukupa kilicho bora. Anataka wewe uingie katika Ufalme
wa Mbinguni; tubu na kuacha uabudu sanamu. Kwasababu ibada ya sanamu haitakuokoa wewe.
Yesu Kristo wa Nazareti ndiye pekee aokoaye, aliyeutoa uhai wake kwaajili yako, yangu na
kwaajili ya wanadamu wote. Bwana ana ujumbe mzito kwa wanadamu. Huku akilia aliniambia,
“Tafadhari, Binti, usikae kimya; nenda na uwaambie ukweli, nenda na uwaambie
nilichokuonesha wewe.”
Sanamu za Maria na Waumini wa kisujudia
Nilimwona Maria akimwabudu Bwana, na niliwaona wanawake wakiwa na nywele ndefu nzuri.
Nikasema, “Bwana, wanapendeza sana walivyoweka nywele zao.” Akaniambia, “Binti, kile
uonacho ni utaji niliowapa wanawake.” Akaongeza, “Binti, nenda na uwaambie wanawake
watunze utaji niliowapa.”
18
Kisha akaniambia, “Nina kitu cha muhimu cha kukuonesha.” Nikatazama mbali kidogo na kuona MJI UNG’AAO, MJI WA DHAHABU! Nikasema, “Bwana, kile ni nini? Nataka kwenda pale.” Akanijibu, “Binti, nitakuonesha kilichopo pale. Ukionacho ni makao ya Mbinguni, majumba ya Mbinguni yaliyotayari kwaajili ya watu wangu.”
Tulianza kutembea, hadi tukafika kwenye daraja la dhahabu. Mara tulipovuka daraja, tukafika kwenye mitaa iliyotengenezwa kwa dhahabu safi! (Ufunuo 21:21)
Kila kitu kilikuwa kizuri sana, kuzuri sana pale, kunang’aa kama kioo, ni mahali pasipo pakawaida, hakuelezeki! Tuliona majumba ya ki-mbinguni na pia tuliwaona, maelfu ya malaika wakijenga. Baadhi ya malaika walikuwa wanajenga kwa haraka ya ajabu, na wengine pole pole na wengine walikuwa wamesimama kabisa kujenga. Nikamuuliza Bwana, “Kwanini malaika wengine wanajenga haraka haraka, wengine polepole, na wengine wamesimama?" Bwana akanieleza, “Binti, hivyo ndivyo wafanyavyo watu wangu duniani, na malaika wanafanya kama wafanyavyo watoto wangu duniani…. Binti, watu wangu hawahubiri neno langu. Watu wangu hawafungi tena. Watu wangu hawaendi mtaani kusambaza ujumbe wa neno langu kwa vipeperushi vinavyoeleza ukweli. Watu wanaona aibu kuhubiri. Nenda kawaambie watu wangu warudi kwenye njia za zamani. Wale malaika uliowaona hawafanyi chochote ni malaika wa watu wangu waliorudi nyuma na kuacha njia zangu… Binti, nenda waambie watu wangu warudi njia zao za zamani,” (Yeremia 6:16) na baada ya kusema haya akaanza kulia Bwana.
Nikasikia watu wengine wakiimba, hivyo nikamuuliza, “Bwana, nataka unipeleke kule, ambako watu wanaimba.” Yesu alikuwa akiniangalia, nakwambia jinsi alivyokuwa ananiangalia, sikuweza kuona vema uso wake bali alikuwa akigeuza uso wake. Wakati huo machozi yalikuwa yakimtiririkia kwenye vazi lake, nikamuuliza kwanini analia. Lakini hakuweza kunieleza.
Baadaye tulifika kwenye bustani nzuri sana. Pale katika majumba ya mbinguni, niliona maua yalikuwa yakiyumbayumba huku na huku kama yapulizwayo na upepo. Hizi huenda ndizo sauti za kuimba nilizozisikia. Bwana akaninyoshea kidole na kusema, “Binti, tazama, maua yananisifu mimi; yananiabudu mimi! Watu wangu hawafanyi hivi tena kama walivyokuwa wanafanya mwanzo. Watu wangu hawanisifu, hawaniiabudu mimi; hawanitafuti mimi kama mwanzo. Ndiyo maana nalikwambia mwanzo, Binti, nenda na uwaambie watu wangu wanitafute, kwa kuwa nitakwenda, nitakwenda, nitakwenda kwa wanaonitafuta kwa roho na kwa kweli, kwa watu walio tayari, kwa watakatifu!” na huku akilia akasema, “Ninakuja, ninakuja!” hapo nikaelewa kwanini alikuwa analia, kwasababu anakuja, lakini si kwa wasio na nia, watu wa nia mbili [vuguvugu]. Atarudi kwa wale tu wanaomtafuta katika roho na kweli.
Ndipo Bwana akaniambia ninatakiwa kurudi duniani. Nikasema, “Bwana, Sitaki kurudi duniani! Unamaanisha nini- duniani? Nataka kubaki na wewe Bwana. Umenileta huku na mimi siendi kokote kwasababu niko na wewe!”
Yesu akasema, “Binti, ni muhimu urudi duniani ili ukashuhudie kwamba utukufu wangu ni halisi, yote niliyokuonesha kuwa ni kweli; ili wanadamu waje kwangu, watubu na wasiangamie.” Bwana akaanza kulia, nami nikaanguka miguuni pake; nikaona vidonda kwenye miguu yake. Nikamuuliza, “Bwana, hivi ni vidonda vya nini?” akajibu, “Binti, ni vidonda ya jana, nilipotoa maisha yangu kwaajili ya wanadamu.”
19
MKONO WA YESU
Bwana akanionesha vidonda vyake vya mikononi, nilimuuliza, “Bwana, kwanini ungalinavyo hata
sasa?” akaniambia, “Binti, ni vidonda vilivyobaki.” Hivyo nikamuuliza, “je vitapona?” akanijibu,
“Vitapona na kufutika tu baada ya watakatifu wote kuungana hapa….. Binti, lazima
nikurudishe duniani: Familia yako na mataifa yanakusubiri wewe.”
Nilijaribu kukataa lakini akanyosha kidole chake chini duniani na kusema, “Tazama, wale watu
uwaonao chini pale ni ndugu zako; na mwili ule uuonao pale, ndiyo utakaoingia…… ni muda
wa kuondoka mahali hapa.” Baada ya hapo akaanipeleka kwenye mto mzuri mwangavu na
akasema, “Binti, ingia katika mto na jizamishe mwenyewe.” Kabla sijaingia ndani ya mto wa maji
ya uzima, nilikuwa najisikia furaha ya ajabu, lakini baada ya kujizamisha na kutoka nje, nilipata
furaha kuu. Nilidhani sitarudi tena nyumbani kwetu, lakini Bwana akaniambia, “Binti, unatakiwa
kurejea duniani….. Binti, nitakuonesha kitu: jinsi nitakavyorudi mara ya pili kwaajili ya watu
wangu watakatifu. Nitakuonesha jinsi siku ile ya kutisha itakavyokuwa.”
FURAHA NA MAOMBOLEZO
Tulitembea hadi sehemu yenye kioo kikubwa kama LUNINGA [TV], nikaona watu. Niliweza
kuona dunia yote. Ghafla nikaona maelfu ya watu wakipotea. Wanawake wenye mimba, mimba
zilipotea, na wakawa kama wamechanganyikiwa na kupiga mayowe.
Watoto walitoweka pande zote. Watu wengi walikuwa akikimbia huko na huku, wakipiga kelele,
“Haiwezekani, haiwezekani, nini hiki kitokeacho?”
Niliwaona wale waliomjua Bwana na kuachwa nyuma. (Mat.24:40-41) Walikuwa wakisema Kristo
amekuja, furaha imetimia. Walikuwa wakipiga kelele na kutafuta kujiua wenyewe lakini
hakuwezekana. Bwana akaniambia, “Binti, siku hizo kifo kitawakimbia; Binti, siku hizo Roho
Mtakatifu hatakuwepo tena.” (Ufunuo 9:6) kulikuwa na ajali nyingi lakini sikuona hata mtu
mmoja aliyekufa: wote walikuwa wazima japokuwa wameumia [majeruhi].
Niliona mlolongo mrefu wa maelfu ya watu. Akaniambia, “Binti, tazama, hivi ndivyo kila kitu
kitakavyokuwa.” Kisha nikaona watu wakikimbia kutoka sehemu moja kwenda nyingine, wakipiga
kelele, Kristo kaja, Kristo kaja!” wakisihi, “Bwana nisamehe mimi, nisamehe mimi, nichukue
nawe!”
20
Baada ya Bwana kuwachukua watu wake [Unyakuo]
Lakini kwa huzuni Bwana akasema, “Watakuwa wamechelewa. Muda wa kutubu ni sasa…. Binti,
nenda kawaambia wanadamu wanitafute mimi, wakati huo hakutakuwa na nafasi. (Isaya 55:6)
Binti, watakuwa wamechelewa wote watakaobakia nyuma.” Baada ya Yesu kuona watu
wataobaki nyuma akaanza kulia na kusema, “Binti, nitakwenda duniani kama neno lisemavyo
katika 1 Thes. 4: 16-17: “Kwasababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na
mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo
watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu,
ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi farijianeni kwa
maneno hayo.”
SIKU YA MWISHO
Lakini si kila mtu atakwenda na Bwana, wale tu wafanyao mapenzi yake (Mathayo 7:21) na aishiye
maisha matakatifu. Kwa kuwa Bwana aliniambia, “Wale tu walio watakatifu wataoingia Ufalme
wa Mbinguni, (Waebrania 12:14) Hakuna ajuaye, siku wala saa nitakayokuja kwaajili ya watu
wangu watakatifu, hata malaika hawajui.” (Mathayo 24:36)
Kwenye Kioo cha LUNINGA [TV] niliona watu wakikimbia huko na huku. Magazeti yalisema
“KRISTO AMEKUJA.” Kioo kikafungwa, na Yesu akamalizia kwa kusema, “Ninakuja kwa
watakatifu.” Hivi ndivyo alivyonionesha mimi. Baada ya hapo akanirudisha duniani hapa. Tukiwa
na kusanyiko la malaika wengi wakituzunguka, tulianza kushuka ngazi nzuri kama nini; ngazi
nyeupe na maua yakizunguka. Nilikuwa nalia njia nzima kushuka chini, nikimsihi Yesu, “Bwana
tafadhari usiniache hapa. Nichukue niwe nawe!” Alinijibu, “Binti, mataifa yanakusubiri,
familia yako wanakusubiri wewe…….. Binti, lazima urejee mwili wako. Lazima upokee uhai
wako, Binti, ili uweze kwenda kushuhudia yote uliyoyaona. Wengi hawatakuamini wewe; wengi
watakuamini, bali mimi ni shahidi wako mwaminifu. Niko pamoja nawe. Sitakuacha kamwe."
21
KURUDI DUNIANI KWA ANGELICA
Maxima:
Binti yangu aliporudi, tulikuwa tunamsubiri pale, na alikuwa amelazwa pale pale chini sakafuni.
Nikasikia mguno, "uuhmm," bila kitu. Nikasema, “ahsante Bwana kwasababu Binti yangu
amerudi!”
Sote tulimshukuru Bwana. Mara akaanza kupumua polepole, kidogo kidogo. Baada ya muda wa
masaa matano, alikuwa na uwezo wa kufumbua macho na kusema. Mwanzo tulipata shida
kumuelewa asemacho; ilikuwa ni vigumu kumuelewa. Hakuwa na nguvu kabisa. Ilibidi tufunge
madirisha kwasababu macho yake hayakuwa na uwezo wa kuhimili mwanga.
Kwakuwa wadadisi, sote tulitaka atueleze alichoona. Lakini kwa kuwa alikuwa dhaifu, aliweza
kutueleza kidogo tu. Ilimchukua karibu wiki mbili hadi alipoweza kutushirikisha habari nzima ya
ushuhuda wake.
Mapepo yalikuja kumtesa baada ya hayo yote. Aliweza kuyaona waziwazi; yalijaribu kujificha
kwenye vivuli. Yalikuwepo hapa karibu siku tatu mfululizo tangu arudi, kabla hajaweza kutueleza.
Aliyauliza yalikuwa yanataka nini, nayo yakamjibu, “tumekuja kufanya mkataba nawe……. Ni
lazima ufunge mdomo, ni lazima usiseme lolote ya hayo uliyaona kule chini, kwasababu ukisema,
tutakuuwa.” Aliyaelezea yalivyo mapepo, yana sura mbaya, makubwa na manene yanatisha.
Alisema hakuna maneno yakuelezea jinsi yatishavyo kwa mwonekano. Alijaribu kuyakemea lakini
yalikataa kuondoka. Yakifika yalikuwa yanamrukia na kumchoma. Naye aliendelea kupambana
nayo na kuyakemea, lakini hakuweza kwasababu hakuwa na nguvu. Siku moja alipokuwa
anayakemea, mwanga mkali wa ajabu ulitokea na yakakimbia yote! Alikuwa ni Bwana.
Alichopitia Binti yangu hakikuwa rahisi. Alipewa ujumbe wenye maono ya ndani kwaajili ya
wanadamu, ili wamtafute Mungu. Wanadamu wanadhani wafanyayo ni sahihi. Vijana wamezama
kwenye madawa ya kulevya na pombe, na kuona ni sawa maisha hayo, lakini si sawa. Miongoni
mwa alioneshwa binti yangu ya kutisha ni wasanii wengi walivyojaa kuzimu, wanamuziki/wacheza
dansi na pia Papa John Paul II. Ni wakati wa kumtafuta Bwana, kutubu, na kujishusha na kujidhiri
mbele za zake. Neno la Mungu ni kweli lisemalo, “Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu
hayatapita kamwe.”(Mark 13:31) Neno la Bwana litatimizwa katika muda wake. Bwana
alimwonesha tanuru ambalo watu walikuwa wanatembea kuelekea kuzimu. Na watu wengi tayari
wakiwakuzimu. Ni kweli haya, lakini hata watu wa Mungu hawaamini haya, wengi hawaamini.
Ujumbe mkuu ni kwamba tumtafute Bwana, siyo kwa kinywa/mdomoni, bali kutoka ndani ya
moyo, kwakuwa kurudi kwa Bwana ku-karibu. Yesu alisema, “Siko tena mlangoni; niko zaidi ya
mlangoni. Nakuja muda simrefu; kuja kwangu ku-karibu. Watu wangu wameniacha na
wamerejea mambo ya duaniani……… waambie watu wangu warudie njia zao za zamani.”
22
Kanisa leo linatakiwa kurudia njia zake za zamani; hapa tulipo ni wa motoni, tumtafute Bwana.
Pale parapanda ikilia tuwe tayari kukutana na Bwana, itakuwa ajabu sana!
UJUMBE WA MUHIMU WA BWANA
Angelica akiongea mbele ya haraiki:
Bwana akaniambia, “Binti, siku hizo Roho Mtakatifu hatakuwepo tena duaniani. Siku hizo
hatakuwepo duniani.” (2 Thes. 2:7) Na nikaona msongamano mkubwa wa magari na ajali nyingi
sana. Watu wengi walijaribu kujiua, lakini Yesu akasema, “Watatafuta kifo, lakini kifo
kitawakimbia wanadamu. Kifo hakitakuwepo tena siku hizo.”(Ufunuo 9:6) Nikawaona watu
wakitazama LUNINGA [TV] na kusoma magazeti yakisema, “Maelfu na maelfu wamepotea.”
Wengi watajua kuwa Yesu ameshakuja kwaajili ya watu wake watakatifu. Wale waliomjua Bwana
lakini wameachwa, wakakimbia mitaani wakilia, wakijaribu kujiua wenyewe lakini hawakuweza
lolote.
Nilipokuwa mbinguni, Yesu alisema, “Nina kuja duniani kwaajili ya watu wangu watakatifu na
ninakuja mapema kwaajili ya kanisa langu.” Lakini wiki mbili zilizo pita Bwana aliniambia,
“Binti, ninafurahishwa na unavyotenda, kwa kuwa unatimiza niliyokuagiza na nakukupa, lakini
usiwaambie watu wangu kuwa nitakuja mapema, waambie ninakuja sasa hivi.” Tena Bwana
akasema, “Waambie watu wangu ninakuja sasa hivi na ninakuja kwa watu watakatifu. Waambie
watu wangu nakuja kwa watakatifu tu, nao ndio wataoniona mimi!.... tena usinyamaze: endelea
kuwashuhudia ninayokwambia.”
Angelica akiomba na haraiki:
Kila mmoja afumbe macho, na weka mkono wako wa kuume kifuani. Inua mkono wa kushoto juu,
kama unajisikia kulia[toba], lia tu. Sasa mweleze Bwana kile unachojisikia moyoni. Kwa wale
waliotayari kumpokea Bwana, wafuatiane nami ktika maneno haya:
Bwana, ninakushukuru kwa Upendo na huruma yako, ahsante Bwana kwa maneno yako
yaliyotufikia mioyoni leo. Baba, ninaomba msamaha kwako, unisamehe. Unisamehe mimi.
Unioshe kwa damu yako ya thamani. Andika jina langu katika kitabu cha uzima. Nipokee/nikubali
mimi niwe mwanao Bwana. Sasa hivi, ninamsamehe kila mtu niliyeshindwa kumsamehe. Ninakana
hali yangu ya kutosamehe. Ninayakana yote yalinizuia nisikufuate Bwana, ninaomba unibadilishe
Bwana na unijaze uwepo wako ndani yangu kila siku. Ahsante Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu,
Ameni.
23
Angelica:
Ushuhuda huu siyo uwongo; siyo mzaha; siyo hadithi; siyo ndoto, kuzimu ni kweli ipo! Kuzimu ni
halisia! Kwa yeyote asiyeamini, nataka kukueleza kuzimu ni kweli ipo, ni kweli ni halisi. Ninakosa
maneno zaidi mazuri ya kuelezea uhalisia wa kuzimu. Natamani kama ungeshuhudia wewe
mwenyewe. Lakini tafadhari amini, tii na uonyeke kwa ushuhuda huu [ushuhuda ukuonye na
kukubadilisha] ili uepuke moto wa milele.
Angelica akiongea na Mfasiri/Muelezeaji:
Muda ukaribu sana, Mungu anaruhusu ishara kwa wanadamu zitokee ili kuwaonesha
kitakachotokea. Usibakie ukihukumiwa; ndilo shetani atakalo. Jiulize kama uko tayari ukitembea
kuelekea shimo la kuzimu? Leo ni siku ya wokovu, leo ni siku ya kumkaribisha Yesu, kuwa Bwana
na mwokozi wa maisha yako. Haya ni maneno rahisi lakini ni makubwa sana kusema: “Ninakubali
na kukupokea Yesu uwe Bwana na Mwokozi wangu. Ninakupa wewe maisha yangu na roho yangu
kwa moyo wangu wote. Natakuwa kuwa nawe kwa maisha ya milele.”
Chagua hatima yako baada ya maisha haya: Uzima au mauti, Mbinguni au kuzimu, Yesu au
shetani. Iko wazi, uko upande wa Yesu au upande wa shetani. Au unafanya yaliyo mema au
unafanya yaliyo mabaya. Chagua mwisho wako: uzima wa milele au ziwa la moto. Fikiria jambo
hili. Fanya uamuzi sasa. Yesu Kristo alikufa msalabani kwaajili yetu, kwa dhambi zetu, na akatupa
fursa ya wokovu kwa huruma yake. Mpokee Yesu Kristo kuwa mwokozi wako!
“Sasa umesikia ushuhuda huu, usiipoteze nafasi hii
ukaijutia milele na milele motoni.”
24
Marejeo:
Ufunuo 19:9 ….Heri walioalikwa karamu ya arusi ya mwanakondoo. ……..maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.
Ufunuo 20:15 Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.
Ufunuo 21:4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwepo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwepo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.
Ufunuo 21:1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
Ufunuo 21:8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
“Hakuna waabuduo sanamu wataourithi ufalme wa Mbinguni.”
Kutoka 20:4-5 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu wenye wivu……..
Ufunuo 21:21 Na milango kumi na miwili ni lulu kumi na mbili; kila mlango ni lulu moja. Na njia ya mji ni dhahabu safi kama kioo kiangavu.
Ufunuo 21:27 Na ndani hakitaingia kamwe chochote kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha mwana koondoo wa Mungu.
Ufunuo 22:7 Na tazama, naja upesi; heri yeye ayashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki.
Ufunuo 22:11 Mwenye kudhuluma na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.
Ufunuo 22:12 Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
Ufunuo 22:13-15 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri ya kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake. Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.
Ndugu aliyefasiri ufunuo huu ni Alpha Wilson Magubila ni Mwana UWATA (Uamusho Wa Wakristo Tanzania); Jumuiya iliyosajiriwa na Yenye Msingi wa Kutubu Dhambi na kuziacha (Mithali 28:13). Waebrania 6:4-6, 2Petro 2:20-22.
Anuani ya Posta: 80405, Dar es Salaam Tanzania, East Africa,
Simu ya Mkononi: +255-754-644559, +255-715-644559.
Barua Pepe: alphawilsonm@hotmail.com
© Blogger template Shush by Ourblogtemplates.com 2009
Back to TOP